NEWS

Thursday 14 November 2019

FAIDA ZA UJENZI WA UWANJA WA SERENGETI


  

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti(DED) Eng Juma Hamsini amesema mapato ya Halmashauri hiyo yanatarajia kuongezeka kutoka shilingi bilioni 3.5 hadi bilioni 10 mara tu ujenzi wa uwanja wa ndege  wa Serengeti utakapokamilika. Tayari ujenzi wa uwanja huo umeanza katika eneo la Burunga nje kidogo ya mji wa Mugumu na unategemea kukamilika 2021.


Aidha Hamsini ameiambia Mara Online News leo kuwa  ujenzi wa uwanja huo wa ndege unalenga pia kuendeleza uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti na kuimarisha ulinzi katika hifadhi ya taifa ya Serengeti na kukuza biashara na uchumi wa wananchi wa kawaida katika mji wa Mugumu na maeneo jirani.

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages