Justine Ogo ambaye ni mwalimu wa shule
ya sekondari Itiryo iliyopo Tarime Mkoani Mara ameuawa leo Novemba 14,2019
asubuhi baada ya kuchomwa mkuki na vijana wanaodaiwa kufanya maandalizi ya
kufanyiwa tohara ya kienyeji.
Taarifa kutoka Itiryo zinasema tayari jeshi la
polisi limewakamata watu kaadha kutokana na mauaji hayo ambayo yamewashitua
walimu na mashirika yanayopinga ukeketaji.
 " Hili ni tukio ambalo limeleta mshituko mkubwa sana hapa  Itiryo. Hao vijana walimchoma mkuki marehemu akiwa kwenye pikipiki akiwa na wenzake wakielekea kusimamia mtihani wa kidato cha pili", amesema mwalimu mmoja wa shule ya msingi ambaye ni mkazi wa kijiji cha Itiryo.
 Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) ambalo linapinga ukeketaji Wilayani Tarime limelaani vikali mauaji ya mwalimu huyo.
" Tumepokea kwa masikitiko makubwa  sana taarifa za mauaji ya  mwalimu wa Itiryo leo asubuhi , leo imekuwa kwake kesho itakuwa mwingine ,", amesema  Juvitus Alphonce ambaye ni Afisa  wa shirika hilo la CDF ofisi za Tarime .
 Juhudi za
Mara Online News kumpata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi TarimeRorya(RPC)SACP Henry
Mwaibambe kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.

 
 
 
 
 
 
.jpeg) 
Mila zingine za kijinga kama hizi zilizopelekea ndugu yetu kupoteza maisha ni vyema zikapigwa marufuku kabisa. Msiba huu umenigusa sana, kiukweli wamekatili sana ndoto za rafiki yangu na mpambanaji mwenzangu.
ReplyDelete