Na mwandishi wetu, Tarime
Jeshi la polisi katika Mkoa wa Kipolisi TarimeRorya limefanikiwa kupata siraha
mbili ambazo moja ni AK47 na ambayo
imetengenezwa kienyeji lakini inatumia risasi za SMG baada ya kukabiliana vikali
na watuhumiwa wa ujambazi katika eneo la Obwere, Shirati Wilayani Rorya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi TarimeRorya Henry
Mwaibambe amewambia waandishi wa habari ofisini kwake leo Novemba 9, 2019 ofisini kuwa
watuhumiwa watatu katika ya watano waliohusika katika tukio hilo
wamefariki dunia.
Pia askari polisi waliokota risasi na maganda ya
risasi kadhaa katika eneo la tukio , amesema kamanda Mwaibambe.
“ Haikuwa kasi nyepesi ilikuwa vita kali na risasi 60 zilizipigwa
katika eneo la tukio”, amesema RPC Mwaimbambe .
Hivi sasa kamanda Mwaibambe amesema wanawasaka
watuhumiwa wawili waliokimbia na siraha aina ya shortgun.
RPC
Mwaibambe amesema siraha ya kienyeji waliopata ina mlio mkali kama wa mabomu .
No comments:
Post a Comment