
Na Mwandishi Wetu
Geita
---------------
Geita
---------------
Wabunge wawili kutoka majimbo ya Chato Kaskazini na Chato Kusini, Cornel Magembe na Paschal Lutandula, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita, James Ruge, aliwambia waandishi wa habari jana kuwa hatua ya kuwafikisha mahakamani wabunge hao inafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa kuhusu tuhuma zinazowakabili.
Sambamba na hao, Ruge alisema madiwani wanne kutoka kata tofauti pia wanashitakiwa kwa tuhuma za kushirikiana na wabunge hao kutekeleza vitendo vya rushwa.
Madiwani hao ni Bartholomeo Manunga, Frank Francis, Josephat Manyenye na Njile Mboligo.
Washitakiwa hao wote wanatuhumiwa kushirikiana kupanga mchakato wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
No comments:
Post a Comment