Balozi wa
Tanzania Nchini Kenya Dr Pindi Chana leo Novemba04,2019 ametia hamasa kubwa na kushuhudia timu ya Copa cocacola Tanzania ikichuana na
timu ya Copa cocacola ya Kenya katika shindano la nusu fainali lilofanyika katika shule ya Mpesa Foundation Academy
nchini Kenya.
Balozi Dr
Pindi Chana amewapongeza vijana wa timu
ya Copa cocacola ya Tanzania kwa kushiriki katika mashindano hayo ambayo fainali
yake itafanyika kesho na kuhusisha pia timu ya Copa Coca cola ya Zimbabwe.
Akiongea na vyombo vya habari katika hafla hiyo,
Balozi Dkt Chana amesema uwekezaji katika michezo kwa vijana sio tu ni muhimu
kwa afya bali pia husadia kutengeneza ajira kwa vijana.
Balozi Dr
Chana pia amezipongeza nchi za Afrika kwa kuweka michezo kuwa sehemu ya masomo
katika shule za sekondari .
No comments:
Post a Comment