Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu jana Januari 24 alikabidhi vitabu vya mipango ya matumzi bora ya ardhi kwa
viongozi wa vijiji 8 na kuwataka viongozi hao kutekeleza mipango hiyo
kikamilifu ili kuondoa migogoro ya ardhi pamoja migogoro kati ya
wanyamapori na binadamu.
Babu pia
alikabidhi kitabu chenye mpango wa matumizi bora ya ardhi wa miaka 20 wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Juma Porini.
Zoezi la
kuandaa mipango hiyo umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani(KfW) na
kuwezeshwa na Shirika la Frankfurt
Zoological Society(FZS) kwa kushirikiana na
Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA).
No comments:
Post a Comment