Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko Jana
Februari 21, 2020 alitembelea ofisi za
Mara Online na kutekeleza ahadi yake
kompyuta ambayo aliahidi mwezi uliopita katika hafla ya uzinduzi wa gazeti la Sauti
ya Mara.
Matiko alipongeza Mara Online kwa kuanzisha gazeti la
Sauti ya Mara ambalo hutoka kila siku ya Jumatatu na kusema gazeti hilo
limeonesha mfano mzuri kwa kuripoti habari ambazo zimejikita zaidi katika maendeleo.
“ Kwa kweli gazeti la Sauti ya Mara ni gazeti ambalo linatoa habari za maendeleo
bila kujali ninani kafanya hayo
maendeleo “, Mbunge huyo alisema.
Aidha mbunge huyo alionesha kukunwa na timu ya
vijana ambao ni wafanyakazi wa Mara Online na kuwaasa kuendelea kufanya kazi kwa
bidii na kuwa na weledi ili waweze kufikia ndoto zao.
Mtendaji Mkuu wa Mara Online Jacob Mugini ambaye ni mwandishi wa habari alimshukuru Mbunge Matiko kwa kuwatembelea na kuwapatia msaada wa kompyuta.
" Mheshimiwa tumefurahi sana kwa kututembelea na umetupa maneno mazuri ya kututia moyo", alisema Jacob
" Mheshimiwa tumefurahi sana kwa kututembelea na umetupa maneno mazuri ya kututia moyo", alisema Jacob
No comments:
Post a Comment