Mkuu
wa Mkoa (RC) wa Mara, Adam Malima, hivi karibuni amefanya ziara katika mwalo wa Sota wilayani
Rorya na kuwataka wavuvi kuwa makini dhidi ya ongezeko kubwa la maji katika
Ziwa Victoria.
Tayari
watu wawili kutoka eneo hilo wanahofiwa kufa maji wakivua samaki ziwani humo.
Hivi
karibuni ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria
(LVBWB) ilitoa tahadhari baada ya kubaini kina cha maji katika ziwa hilo
kimeongezaka hadi kufikia mita 1134.47 kutoka usawa wa bahari.
Watalaamu
wanasema kiwango hicho cha maji kimevunja rekodi kwani hakijawahi kufikiwa
katika kipindi cha miaka 55 iliyopita.
Aidha, Mkuu wa Mkoa, Malima, ametawaka wavuvi kutotumika kuvusha wageni kuingia nchini kiholela, hasa kipindi hiki cha mlipuko wa janga la COVID-19 linalosababishwa na virusi vya corona.
Amewandoa
hofu wavuvi hao dhidi ya vitendo vya utekwaji wakiwa katika shughuli zao
akisema serikali itaendelea kuimaisha doria katika ziwa hilo.
Lakini ametawaka kufanya uvuvi upande wa Tanzania na kuacha tabia ya kuvuka mipaka.
Ziwa
Victoria linazungwaka na nchi tatu za Afrika Mashariki; ambazo ni Tanzania, Uganda
na Kenya.
(Habari,
picha zote na Mussa John, Rorya)
No comments:
Post a Comment