Watu watatu wakiwemo wanawake wajawazito wawili
wamekufa maji ndani ya Mto Mara walipokuwa wanavuka kutoka kijiji cha Borenga
Wilayani Serengeti kwa mtumbwi wakielekea Nyamongo Wilayani Tarime.
“ Hili tukio lilitokea juzi asubushi na mtumbwi huo ulikuwa na watu saba na wanne
wameokolewa lakini watatu wamefariki
dunia”, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu aliiambia Mara Online News kwa
njia ya simu leo asubuhi
Mkuu huyo wa Wilaya amepiga marufuku matumizi ya
mitumbwi katika maeneo jirani yaliyo na mto Mara kutokana na mto huo na mito
mingine kujaa maji hivi sasa.
No comments:
Post a Comment