Mamlaka ya dawa na chakula nchini Marekani (FDA) imetoa ruhusa ya dharura ya dawa ya Ebola inayofahamika kama 'remdesivir' kutumika kuwatibia wagonjwa wenye virusi vya corona.
Ruhusa ya kutumika kwa dawa hiyo kwa sasa imetolewa kwa watu ambao wamelazwa hospitalini tu kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
Jaribio la hivi karibuni la kitabibu linaonyesha kuwa dawa hiyo inaweza kuwasaidia watu mahututi wanaoumwa corona, na inaaminiwa kuwa inaweza kuwasaidia kupona haraka.
Hatahivyo, haijaonyesha kuwa inasaidia kupunguza idadi ya vifo.
Wataalamu wa dawa wametoa onyo kuhusu dawa hizo -ambazo zilitengenezwa ili kutibu Ebola, na zilitengenezwa na kampuni ya Gilead pharmaceutical iliyopo mjini California -kwamba visionekane kuwa ni jambo la ajabu sana kwa dawa hiyo kuanza kutumika kwa ajili ya kutibu virusi vya corona.
Dawa hiyo inaweza kuigwa na kuharibu utendaji wake.
Katika kikao na rais wa Marekani Donald Trump katika ofisi za Oval, Mkurugenzi mkuu wa Gilead Daniel O'Day alisema Mamlaka ya dawa FDA ndio hatua muhimu ya kwanza.
Kampuni hiyo itachangia chupa za dawa hiyo milioni 1.5 , alisema.
Kamishina wa FDA, bwana Stephen Hahn alisema kwenye mkutano huo: "Hii itakuwa tiba ya kwanza ya Covid-19 kupitishwa , tumefurahi sana kuwa sehemu ya uwezeshaji huo."
Mamlaka ya dharura ya FDA si sawa na ile ambayo inatoa idhini rasmi ambayo inahitaji uangalizai wa hali ya juu zaidi.
BBC Swahili
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment