Misiwa
ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyamwaga, bila shaka atachuana na mbunge wa
jimbo hilo anayemaliza muda wake, John Heche, miongoni mwa makada wengine wa
chama hicho watakaojitokeza kuomba nafasi hiyo.
Katika
mazungumzo yake na Mara Online News
hivi karibuni, Misiwa amesema anaamini kwamba kitakachombeba katika
kinyang’anyiro hicho ni maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya yaliyopatikana chini
ya uongozi wake kama mwenyekiti.
Misiwa akizungumza katika moja ya mikutano wa ziara ya viongozi na wananchi |
Elimu ilivyopaishwa
Misiwa
amesema elimu ni miongoni mwa sekta zilizopata mafanikio makubwa katika kipindi
cha uongozi wake kama mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
“Tuanze
na elimu ya msingi, kwa mara ya kwanza halmashauri yetu imeanzisha shule mpya
zaidi ya shule 10. Haya ni mfanikio makubwa katika kuhakikisha watoto wetu
wanapata elimu ambayo ni ufunguo wa maendeleo katika jamii yoyote,” amesema.
Misiwa
emetaja baadhi ya shule hizo kuwa ni Maika, Nyamiri na Makerero.
Kwa
mujibu wa Misiwa, halmashauri hiyo imetumia Sh zaidi ya milioni 700 kutengeneza
madawati 1,200 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi, hivyo kufanya tatizo
lililokuwepo kubaki historia.
“Kwa
sasa hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa dawati katika halmashauri yetu
na tumefanikiwa haya yote kwa kutumia mapato ya ndani,” amefafanua Misiwa.
Ameongeza
kuwa halmashauri pia imetumia Sh bilioni 1.4 kugharimia ukamilishaji vyumba vya
madarasa katika shule za msingi na sekondari 150.
Kwa
upande wa elimu ya sekondari, amesema halmashauri imeweza kujenga shule mpya za
sekondari tano; ambazo ni Muriba, Ganyange, Nyansisine na Kewamamba. Katika
kata ya Kiore zimejengwa shule mbili.
“Shule
hizi mpya zimepokea shilingi zaidi ya milioni 200,” amesema.
Afya
yamwagiwa mamilioni
Kwa
upande wa sekta ya afya, Misiwa amejivunia ujenzi hospitali mpya ya halmashauri
iliyopo Nyamwaga yalipo makao makuu ya halmashuri hiyo.
“Wote
ni mashahidi kuwa ilianza kama zahanati na sasa ni hospitali ya halmashauri ya
wilaya na tulipitisha shilingi milioni 300 kwa ajili ujenzi na ununuzi wa
vifaa, jambo ambalo lilisaidia kuifanya hospitali hiyo kupata usajii na inatoa
huduma kwa wananchi wetu,” amefafanua.
Misiwa
ametumia nafasi hiyo pia kuwashukuru viongozi wa serikali ambao wamekuwa
wakishirikiana kwa karibu katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo wa
hospitali.
Aidha,
amesema halmashauri hiyo imeweza kuboresha upatikanaji wa huduma katika vituo
vya afya.
Wananchi wakipata huduma katika Hosptali mpya ya Tarime DC |
Vituo
vingine vya afya ni Sirari (Sh milioni 600) kutoka Serikali Kuu na halmashauri,
Kiongera (Sh milioni 80), Mtana (Sh milioni 80) na Nyarwana (Sh milioni 200).
“Upande
wa zahanati ni nyingi, lakini nitaje tu Ganyange, Kimusi na Itiryo ambapo tumepeleka
shilingi milioni 320,” amesema mwenyekiti huyo wa halmashauri.
Barabara
zilivyoboreshwa
Misiwa
amesema uwekezaji mkubwa ulielekezwa pia katika kuboresha miundombinu ya
barabara ambapo nyingi zilizokuwa hazipitiki sasa zinapitika.
Misiwa akihakikisha kuwa ujenzi wa barabara unaenda sawa |
“Mfano
tumezibua njia mpya nyingi kuanzia Nyamwaga – Magoto au Misiwa road, Bikonge -
Custom, Mangucha - Nyandage, Taisi - Matamankwe na Bumera – Susuni,” amesema
Misiwa na kuongeza:
“Tumetumia
mapato ya ndani kuboresha barabara Nyamwaga – Nyanungu yenye urefu wa kilomita
1.5 kwa kiwango cha lami. Pia tumejenga barabara ya Nyamwaga Escarpment –
Nyamogo kupitia Kasco kwa kiwango cha lami, hizi zote hazikuwepo.”
Misiwa
anaamini wananchi hawatamwangusha katika kinyang’anyiro cha ubunge Tarime
Vijijini, hasa ikizingatiwa kuwa usimamizi wake thabiti kama mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ndio umefanikisha miradi hiyo na mingine mingi kwa
manufaa ya umma.
Mikopo
kwa vijana, wanawake
Misiwa
anasema halmashauri hiyo katika mwaka 2014/2015 ilielekeza mkopo wa Sh milioni
36 kwa vikundi vya vijana na wanawake.
“Kwa
mara ya kwanza mwaka 2015/2016 nimehakikisha shilingi zaidi ya bilioni 1.2 zinatolewa
kwenda kwa vikundi vya vijana na wanawake”, anaongeza Misiwa.
Hati safi
halmashauri
Kwa
upande mwingine, Misiwa anasema katika kipindi cha uongozi wake, Halmashauri ya
Wilaya ya Tarime imeendelea kupata hati safi kutoka kwa Mthibidi na Mkaguzi wa
Hesabu za Serikali (CAG).
Misiwa akionesha hati safi |
Kwanini anataka
ubunge?
Misiwa
anasema akipata nafasi ya ubunge atawaletea wananchi wa Tarime Vijijini
maendeleo makubwa zaidi ya aliyowezesha akiwa mwenyekiti wa halmashauri na
diwani.
Misiwa(kulia) kulia akiongoza kikao cha baraza la madiwani |
(Habari, picha na Mara Online news)
No comments:
Post a Comment