NEWS

Tuesday 5 May 2020

NEMC yatoa siku 30 wachimbaji wadogo wajisajili

Mkugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt Samuel Gwamaka


BARAZA la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limetoa siku 30 kwa wachimbaji wadogo wote wenye mitambo ya kuchenjua na kuchoma madini kuhakikisha wanajisajili kwenye baraza hilo.

Hatua hiyo ya NEMC imekuja siku chache baada ya kuripotiwa kwa vifo vya mifugo katika maeneo ya wachimbaji wadogo katika wilaya za Tarime na Geita.

Mkugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt Samuel Gwamaka (pichani), ametoa agizo hilo Jumatatu Mei 4, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

“Baraza linawaekeleza wote wenye miradi ya kuchenjua madini, wanoachimba madini, wanaochoma dhahabu (elusion)  wajisajili na baraza ndani ya siku 30,” amesema Dkt Gwamaka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages