DIWANI
wa Kata ya Mbalibali wilayani Serengeti, John Ng’oina (CCM), amefariki dunia
Alhamisi Mei 7, 2020 nyumbani kwake mjini Mugumu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mhandisi Juma Hamsini,
amezungumza na Mara Online News leo Ijumaa Mei 8, 2020 asubuhi na kuthibitisha
kifo hicho.
“Huyu
mzee bwana amefariki jana [Alhamisi] nyumbani kwake usiku na tunaendelea
kuwasiliana na familia kuhusu namna bora ya mazishi ili kumpuzisha maana ni mtu
wa watu, sio tu kutoka Serengeti bali ndani na nje ya Tanzania,” amesema
Mhandisi Hamsini.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi huyo, Ng’oina amekuwa akisumbuliwa na tatizo la figo kwa
miaka kadhaa sasa na amekuwa akipata matitabu nchini India mara kwa mara.
Ng’oina
amekuwa kada mkongwe wa CCM, ambaye amepata kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Serengeti kwa miaka mingi na alitumia nafasi hiyo kuanzisha miradi mikubwa ya
maendeleo katika sekta za elimu na afya.
John Ng'oina akiendesha kikao cha madiwani enzi za uhai wake |
Ng’oina
atakumbukwa pia kwa juhudi zake za kuanzisha ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya
ya Serengeti ambayo sasa imeanza kutoa huduma kwa wananchi baada ya Serikali ya
Awamu ya Tano kutoa Sh milioni 800 kugharimia ukamislishaji wa baadhi ya
majengo muhimu ya hospitali hiyo.
Aidha,
Ng’oina alikuwa mmoja wa viongozi waliopigia debe ujenzi wa uwanja wa ndege
Mugumu ambao maandalizi yake yamefikia hatua nzuri.
No comments:
Post a Comment