MWANAMKE mlinda amani kutoka Brazil
anayehudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na mlinda amani mwanamke kutoka
India ambaye amehitimisha hivi karibuni jukumu lake nchini Sudan Kusini,
wamechaguliwa kupokea Tuzo ya Mwaka 2019 ya Umoja wa Mataifa (UN) ya mwanajeshi
mchagizaji wa masuala ya kijinsia.
Washindi hao, Kamanda Carla Monteiro
de Castro Araujo, Afisa wa Jeshi la Anga la Brazili ambaye kwa sasa anahudumu
kwenye mpango wa Umoja wa Matafa wa kurejesha utulivu nchini Jamhuri ya Afrika
ya Kati (MINUSCA) na Meja Suman Gawani kutoka
Jeshi la India, mwanajeshi mwangalizi wa zamani wa mpango wa Umoja wa Mataifa
nchini Sudan Kusini (UNMISS), walipokea tuzo hiyo wakati wa hafla iliypfanyika
mtandaoni ikiendeshwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kuadhiisha Siku
ya Kimatafa ya Walinda Amani Ijumaa Mei 29, mwaka huu.
Tuzo
ya Jinsia ya UN
Tuzo hiyo “Mwanajeshi mchagizaji wa
mwaka wa masuala ya kijinsia” iliyoanzishwa mwaka 2016, inatambua kujitolea
na juhudi za mwanajeshi mlinda amani katika kuchagiza misingi ya azimio namba
1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, amani na
ulasalma katika muktadha wa operesheni za amni, wakipendekezwa na wakuu au
makamanda wa operesheni za ulinzi wa amani.
Kwa mara ya kwanza, wanawake hao
walinda amani walipokea tuzo hiyo kwa pamoja kwa mchango wao katika suala hilo
muhimu.
Baada ya kupokea taarifa za ushindi
huo, Kamanda Monteoro de Castro Araujo alisema “Tuzo hii ni utambuzi
wa kazi inayohusisha kikosi cha MINUSCA na kitengo cha raia. Ni jambo la kufurahisha
na kuridhisha kwangu mimi na kwa mpango mzima kuona kwamba miradi yetu inazaa
matunda.”
Naye Meja Gawani alielezea faraja
yake kwa kuona kazi yake kama askari mwangalizi wa Umoja wa Mataifa
imetambuliwa.
“Kwa majukumu yetu yoyote, msimamo wetu au cheo chetu ni jukumu letu
kama walinda amani kujumuisha mtazamo wa jinsia zote katika kazi yetu ya kila
siku na kuumiliki, katika muingiliano na wafanyakazi wenzetu, pamoja pia na
jamii,” alisema Meja Gawani.
Kamanda
Monteiro
Kamanda Monteiro de Castro Araujo
amehudumu kama mwanajeshi mshauri wa jinsia na ulinzi katika vikosi vya
MINUSCA makao makuu tangu Aprili 2019.
Wakati wa muhula wake alianzisha na
kuendesha mafunzo ya kina katika masuala yanayohusiana na jinsia na ulinzi.
Kupitia juhudi zake, mpango huo
uliongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wasimamizi wa masuala ya jinsia na ulinzi
na vituo pia.
Pia alikuwa chachu muhimu katika
kushuhudia doria za hatua zinazohusisha masuala ya jinsia zikihusisha jamii na
kukiongezeka kutoka 574 hadi kufikia karibu 3,000 kwa mwezi.
Meja
Gawani
Tangu kupelekwa kwake UNMISS Desemba
2018, Meja Gawani amefundisha waangalizi zaidi ya 230 wa Jeshi la Umoja wa
Mataifa (UNMO) kuhusu ukatili wa kingono unaohusiana na vita na kuhakikisha
uwepo wa waangalizi wanajeshi wanawake katika kila timu ya vituo vya mpango
huo.
Kwa kutoa msaada, ushauri, mwongozo
na uongozi, Meja Gawani alisaidia kuunda mazingira ya kuwezesha walinda amani
wa Umoja wa Mataifa.
Pia alifundisha vikosi vya Serikali
ya Sudan Kusini na kuwasaidia kuzindua mpango mkakati wao wa kukabiliana na
ukatili wa kingono uliohusiana na vita.
Hongera
kwa kazi nzuri
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Antonio Guterres, aliwapongeza Kamanda Monteiro de Castro Araujo na Meja Gawani
kwa tuzo zao.
“Walinda amani hawa ni mfano wa
kuigwa, kupitia kazi zao wameleta mitazamo mipya na wamesaidia kujenga imani na
ujasiri katika jamii tunazozitumikia.” alisema Katibu Mkuu huyo na kuongeza:
“Kupitia kujitolea na njia zao za
ubunifu wamekumbatia kiwango cha ubora ambacho ni msukumo mkubwa kwa walinda
amani wote kila mahali. Tunapokabiliana na changamoto za sasa kazi yao
haijawahi kufaa au kuwa na umuhimu zaidi kama wakati huu.”
Huu ni mwaka wa pili mfululizo
mlinda amani kutoka Brazil anapokea tuzo hiyo ya heshima na ni mara ya kwanza
tuzo hii kwenda kwa mlinda amani kutoka India.
Washindi wa Tuzo ya Masuala ya Jinsia ya UN Mwaka 2019, Meja Suman Gawani (Kushoto) wa Jeshi la India aliyetumika awali UNMISS na Kaman Carla Monteiro de Castro Araujo, Afisa wa Jeshi la Anga la Brazil ambaye sasa anafanyakazi na MINUSCA.
|
No comments:
Post a Comment