NEWS

Sunday 23 August 2020

Kembaki mguu sawa ubunge Tarime Mjini

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Mjini, Elias Ntiruhungwa (kushoto), akimkabidhi Michael Kembaki fomu ya NEC ofisini kwake leo asubuhi
 

MTEULE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Michael Kembaki, leo Jumapili Agosti 23, 2020 amechukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kugombea ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini mkoani Mara.

Michael Kembaki (katikati) akisindikizwa kwenda kuchukua fomu ya NEC. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tarime, Godfrey Francis na baadhi ya makada wa chama hicho
 

Kulingana na duru za siasa, Kembaki anatarajiwa kuleta ushindani mkali dhidi ya Esther Matiko wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayetetea kiti hicho.

Michael Kembaki akiwafungia wakazi wa Tarime Mjini wakati akielekea ofisi ya Msimamizi wa Uhaguzi Jimbo la Tarime Mjini kuchukua fomu za NEC leo asubuhi
 

Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani zitaanza Agosti 26, 2020 nchini kote na uchaguzi wenyewe utafanyika Oktoba 28, 2020.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages