Mgombea ubunge jimbo la Bariadi kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, Erasmus Ndege Lilanga |
MGOMBEA
ubunge jimbo la Bariadi kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, Erasmus Ndege Lilanga
ambaye ni Makamu Askofu wa Kanisa la Spritural Church of Pentecost of
Tanzania Kanda ya Mashariki mwa Ziwa ikiwemo mikoa ya Simiyu na Shinyanga,
amesema akichaguliwa atakuwa mwepesi wa kutatua changamoto zote kwa wakati.
Lilanga amezitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni pamoja na tembo kuvamia mashamba
na makazi ya watu ambapo amesema akifanikiwa kuchaguliwa ataweka msukumo
serikalini ili litatuliwe haraka.
"Ndugu yangu mwana Bariadi, mimi na wewe tumejionea kwa macho tembo
wanavyovamia mashamba na makazi yetu na kuyaharibu kabisa, hivyo nawashauri
tena na tena nipeni ridhaa yenu mnichague niwawakilishe katika kuwatetea na
kuitaarifu serikali yetu kwa njia mbalimbali bungeni na hata kwa maandishi
ikibidi,” amesema jana mara baada ya uzinduzi wa kampeni zake kwenye eneo la
stendi ya zamani ya mabasi iliyopo mjini Bariadi, Simiyu.
Erasmus Ndege Lilanga |
Mbali na hilo, Lilanga amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anakutana na
maafisa kilimo wilayani hapa kuona namna bora ya kuboresha kilimo ambacho
kitamkwamua mkulima kwa kulima mazao yanayouzika (yenye soko) na hivyo kupata
tija kwenye kilimo.
Mgombea huyo ametaja vipaumbele vyake vitano kuwa ni imani juu ya uwepo wa
Mungu itawale, amani ya Mungu itawale, ukweli wa Mungu utawale, umoja wa
Mungu utawale na agizo la Mungu kila mtu afanyekazi litawale.
Aidha, Lilanga ameahidi kuendelea na kampeni kwa kunadi sera za chama chake na vipaumbele
vyake huku akitaja kaulimbiu ya chama hicho kuwa ni "NCCR Mageuzi, utu,
itikadi yetu".
(Imeandikwa na Anita Balingilaki, Bariadi)
No comments:
Post a Comment