NEWS

Tuesday 1 December 2020

Kemanyanki yabeba Siku ya Ukimwi Duniani 2020 mkoani Mara

Mkurugenzi wa Kemanyanki Group, Nicolaus Mgaya, akizungumza na Mara Online News wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Nyamongo wilayani Tarime leo.

 

KIKUNDI cha Kemanyanki maarufu kwa jina la Kemanyaki Group, kimeandaa na kuratibu kwa mafanikio maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani katika mkoa wa Mara - yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Nyamongo wilayani Tarime, leo Desemba 1, 2020.

Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Nyamongo wilayani Tarime.


 

Mkurugenzi wa Kemanyanki Group, Nicolaus Mgaya, amesema mafanikio hayo ni matunda ya ushirikiano thabiti wa wafanyakazi wa kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka na nusu uliopita – kikifanya kazi chini ya ufadhili wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo wilayani Tarime – Mara, ambao kwa sasa unaendeshwa kwa ubia wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Kimataifa ya Barrick na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wananchi wakiwa katika msururu wa kupata huduma ya kupima ili kujua afya zao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Nyamongo wilayani Tarime.

 

Mgaya amesema Kemanyanki Group kinajishughulisha na usafi wa mazingira, ujasiriamali – ukiwemo ufugaji kuku na nguruwe, biashara ndogondogo na ukandarasi katika mgodi wa North Mara, huku akiweka wazi kwamba hadi sasa kimeshawezesha ajira kwa vijana 150 – wengi wao wakitoka kata tano zenye vijiji 11 vilivyo jirani na mgodi huo.

 

#Mara Online News

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages