NEWS

Thursday 3 December 2020

Mwera Mwenyekiti mpya Hospitali ya Tarime

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri (aliyesimama) akihimiza jambo wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Usimamizi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

 

MKUU wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Mhandisi Mtemi Msafiri, amesimamia uchaguzi wa viongozi na kuzindua Kamati ya Usimamizi wa Hospitali ya Wilaya hiyo.

 

Shughuli hizo zimefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Tarime, jana Desemba 2, 2020 ambapo pia zimehudhuria na viongozi wa afya akimwemo Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt Calvin Mwasha.

 

Mwasisi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation, Peter Mwera amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Mchungaji John Maguge wa KKKT Usharika wa Tarime.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Peter Mwera (aliyesimama) akiomba usirikiano kwa wajumbe wenzake baada ya kuchaguliwa. Waliokaa ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri (kushoto) na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt Calvin Mwasha (wa tatu kutoka kushoto).

 

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Bertha Rwebwembela, Mary Samson, Mchungaji Thomas Ryoba, Bhoke Mhono na Mgaya Isaya – ambao wameteuliwa kwa kuzingatia mwongozo wa uundaji wa kamati za vituo vya afya wa mwaka 2013.

 

Aidha, kwa mujibu wa mwongozo huo, wajumbe wengine wanne wanaingia moja kwa moja kwenye vikao vya kamati hiyo kwa nafasi zao.

 

Wajumbe hao ni Joseph Ninga (mwakilishi wa timu ya uendeshaji wa huduma za afya wilayani), Jonia Kafuruki (mwakilishi wa ofisi ya Halmashauri/Mkurugenzi), Dkt Innocent Kweka (Mganga Mfawidhi wa Hospitali atakayekuwa Katibu wa Kamati) na Mkami Mirumbe (Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali).

Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime katika kikao chao cha uchaguzi na uzinduzi.

 

Kamati hiyo, kwa mujibu wa mwongozo, itatakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu.

 

Katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Msafiri, ameitaka kamati hiyo kusimamia hospitali hiyo kwa weledi iwe kimbilio la wananchi kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu.

Sehemu ya mojawapo ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

 

Naye Mwenyekiti Mwera, amewaomba wajumbe wa kamati hiyo kumpatia ushirikiano wa dhati waweze kusaidia kusimamia uboreshaji wa huduma za hospitali hiyo.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages