NEWS

Friday 18 December 2020

Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya afariki dunia

 

Chanzo cha Chanzo cha familia kimesema Bwana Buyoya alifariki dunia mjini Paris, Ufaransa
Maelezo ya picha,

Pierre Buyoya alihudumu mihula miwili ya urais kwa mapinduzi

Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya amefariki akiwa na umri wa miaka 71 ,binamu yake na chanzo cha kidiplomasia chathibitishia BBC.

Chanzo cha familia kimesema alifariki mjini Paris, Ufaransa siku ya Alhamisi kutokana na athari za ugonjwa wa Covid-19.

Jenerali huyo mstaafu alihudumu mara mbili madarakani kwa jumla ya miaka 13 baada ya kumpindua watangulizi wake madarakani

Mwezi Oktoba, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama ya Burundi kwa kosa la mauaji ya rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini, Rais Melchior Ndadaye mwaka 1993 - ambayo yalisababisha mauaji ya karibu watu 300,000. Alikana kufanya makosa

Mwezi uliyopita, alijiuzulu kama mjumbe wa Muungano wa Afrika wa eneo la Sahel, na kusema kuwa anataka kutumia muda wake zaidi kusafisha jina lake.

Maisha ya Buyoya katika siasa za Burundi

Marehemu Pierre Buyoya aliingia madarakani kwa mwara ya kwanza kama rais baada mapundizi ya kijeshi dhidi ya utawala wa rais Jean-Baptiste Bagaza mwaka 1987 ambaye pia aliingia madarakani kwa mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake Michel Micombero mwaka 1976.

Utawala wake wa miaka sita uligubikwa na mambo mbali mbali ambayo yalibadili sura ya nchi kama vile mauaji ya kinyama yaliyofanyika katika kitongoji cha Ntega-Marangara mwaka 1988, makubaliano ya umoja wa Warundi yaliyoidhinishwa mwaka 1991, kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1993, na mengine mengi.

Aliondoka madrakani mwaka 1993 baada ya kushindwa katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kuwahi kufanyika tangu mwaka 1960. Wakati huo , mtangulizi wake Prezida Melchior Ndadaye kutoka chama cha Frodebu ndiye aliyemshinda kwa asilimia zaidi ya 65% ya kura na Pierre Buyoya aliyekuwa wakati huo amegombea kwa tiketi ya chama cha Uprona aliibuka na 33% za kura.

Buyoya alirejea tema madarakani mwezi wa Julai 1996, baada ya kumpindua tena madarakani rais wa mpito Sylvestre Ntibantunganya, ambaye wakati huo alichukua madarakan kufuatia kifo cha Cyprien Ntaryamira yambaye alikufa katika ajali ya ndege pamoja aliyekuwa rais wa Rwanda wakati huo Juvenal Habyarimana.

Rais Ntaryamira alikuwa ameshikilia kiti cha urais kwa miezi miwili pekee, baada ya kifo cha Rais Ndadaye.

Kuuawa kinyama kwa Rais Ndadaye kulilitumbikiza taifa katika vita vya kikabila , kati ya Watusi na Wahutu nchini humo.

Utawala wa rais Buyoya ulitawaliwa na mzozo wa kikakabila baina ya Watutsi na Wahutu
Maelezo ya picha,

Utawala wa Buyoya ulitawaliwa na mzozo wa kikakabila baina ya Watutsi na Wahutu

Hali hiyo ilimlazimu Rais Buyoya kufanya mazungumzo na wapinzani wa serikali waliokuwa wameanzisha vita , mazungumzo yaliyodumu kwa muda wa miaka miwili kuanzia mwaka 1998 hadi panede hizo mbili zilipoweza kusaini makubaliano ya amani mwezi Agosti mwaka 2000.

Tangu wakati huo , Rais Buyoya alikubaliwa kuhudumu kwa kipindi cha mpito cha kilichokubaliwa katika makubaliano ya kwanza kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyoidhinishwa Arusha, na baadaye akaondoka madarakani mwaka 2003 na utawala wa nchi kuchukuliwa na Rais Domitien Ndayizeye.

Mwaka 2008, aliteuliwa kuwa mjumbe maalumu wa amani Umoja wa Mataifa katika nchi ya Mali na Sahel kufuatia mzozo wa kivita uliokuwa ukitokota kati ya Mali na nchi jirani ya Sudan.

Mwezi wa Januari mwaka 2013, ndipo aliteuliwa tena na Umoja wa Afrika kama mjumbe maalumu katika nchi ya Mali na eneo la Sahel.

Pierre Buyoya alikuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika katika nchi ya Mali na eneo la Sahel
Maelezo ya picha,

Pierre Buyoya alikuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika katika nchi ya Mali na eneo la Sahel

Mwaka 2014, alijaribu kugombea nafasi ya uongozi wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa na wakati huo serikali ya Burundi ilimuunga mkono kwani uhusiano baina yao ulikuwa bado ni mzuri.

Hatahivyo mambo yalibadilika kuanzia mwaka 2015,wakati ulipoibuka mzozo wa kisiasa kuhusiana na aliyekuwa rais wa Burundi hayati Pierre Nkurunziza, kugombea muhula wa tatu wa urais.

Wakati huo wapinzani wa serikali walisema kuwa hatua ya Nkurunziza ni kinyume cha sheria , lakini chama chake cha CNDD-FDD, walisisitiza kuwa hatua hiyo ni kwa mujibu wa sheria.

Bw Buyoya hakukubaliana na hatua ya Nkurunziza kugomea urais kwa muhula wa tatu akinukuu kuwa "makubaliano ya amani ya Arusha'' yanabainisha wazi kwamba rais anapaswa kuongoza kwa mihula miwili pekee.

Kutokana na kauli hiyo, uhusiano wake na utawala wa Nkurunziza uliharibika na hakuweza tena kukanyaga katika ardhi ya Burundi.

Uhusiano baina ya Buyoya na Nkurunziza uliingia dosari wakati Buyoya alipopinga hatua ya Nkurunziza kuwania muhula wa tatu madarakani
Maelezo ya picha,

Uhusiano baina ya Buyoya na Nkurunziza uliingia dosari wakati Buyoya alipopinga hatua ya Nkurunziza kuwania muhula wa tatu madarakani

Mwishoni mwaka 2018, Buyoya aliwekwa katika orodha ya watu 17 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya Rais Melchior Ndadaye.

Buyoya hakutarajia hilo kwani alitarajia kuwa makubaliano ya Arusha yatamlinda, ambayo alisema kuwa suala la mauaji ya Ndadaye litachunguzwa na mahakama kubaini ukweli kuhusu mauaji hayo. Buyoya alisema kuwa kesi hiyo ina misingi ya kisiasa.

Alisema kuwa uchunguzi wa kifo hicho unaweza kuibua ghasia za ubaguzi wa kikabila.

Hilo halikuizuia mahakama kumhukumu kifungo cha maisha jela pamoja watu wengine 16 waliopatikana na hatia ya mauaji ya , Melchior Ndadaye , hukumu iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka huu

Buyoya na wenzake walisema kuwa watakata rufaa dhidi uamuzi huo wa mahakama

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages