NEWS

Saturday 16 January 2021

Mabadiliko ya WhatsApp: Signal yagoma kufanya kazi baada ya kupata watumiaji wapya kwa kasi

 Mtandao wa kijamii wa Signal umetangaza kukumbwa na ''matatizo la kiteknolojia'' siku ya Ijumaa wakati likiwapokea watumiaji wapya.


Baadhi ya watumiaji wa mtandao huo wanashindwa kutuma ujumbe katika simu zao za mkono au kwenye komputa kwa saa kadhaa.

Kampuni ya Signal imeshuhudia ongezeko kubwa la watumiaji baada ya WhatsApp kuzindua sheria mpya ya faragha.

Katika mtandao wa Twitter, Signal imesema imeongeza uwezo wa kuweza kuwahudumia watumiaji zaidi.

"Mamilioni ya watumiaji wapya wanatuma ujumbe ambao ni wa siri ," alisema kwenye Tweeter.

1px transparent line

Signal pamoja na Telegram, ambazo ni programu nyingine ya ujumbe mfupi zimefaidika baada ya WhatsApp kuboresha masharti na taratibu zake.

WhatsApp inasemekana kuwa na watumiaji bilioni mbili ambao wanalazimika kushirikisha taarifa zao kwa kampuni mama ya Facebook kama wanataka kuendelea kutumia mtandao huo.

Masharti hayo hayawahusishi watumiaji wa Uingereza na Ulaya tu - lakini taarifa hiyo inatumwa kwa kila mtu.

WhatsApp imefafanua kuwa hatua ya kushirikisha taarifa za mtu binafsi na mtandao wa Facebook si mpya, na haujaongezwa lolote.

Kumekuwa na mkanganyiko kuhusu ujumbe ambao unawataka watu kukubali masharti hayo mpaka ifikapo Februari 8 au kuacha kutumia huduma hiyo.

Whatsapp sasa imebadilisha tarehe ya kuzima mpaka Mei 15, wakisema wameongeza muda ili kuwaelewesha watu vizuri kwa kuwa hawakuwa wameielewa taarifa waliyotoa.

"Hatuwezi kuona ujumbe wa siri au kusikiliza simu za siri na hata Facebook haiwezi kufanya hivyo," Whatsapp iliandika kwenye blog ya FAQ.

Kwa mujibu wa data zilizoelezewa na taasisi ya Sensor Tower, Signal ilipakuliwa mara 246,000 duniani kote wiki kabla ya WhatsApp kutangaza mabadiliko Januari 4 na wiki iliyofuata watu milioni 8.8.

Nchini India, watu waliopakuwa programu hiyo walikuwa 12,000 mpaka milioni 2.7. Uingereza walikuwa 7,400 mpaka 191,000, na Marekani kuanzia 63,000 mpaka milioni 1.1.

Jumatano, Telegram ilisema ilipata watumiaji milioni 500 duniani kote. Na watu waliopakuwa programu hiyo iliongezeka mpaka milioni 6.5 kwa wiki kuanzia Desemba 28 mpaka milioni 11 kwa wiki iliyofuata.

Wakati huo huo, watu waliokuwa wakiipakua program ya WhatsApp ilishuka kutoka milioni 11.3 mpaka milioni 9.2.

Ni kitu gani WhatsApp inaishirikisha Facebook?

WhatsApp ilisema taarifa ya mtumiaji inayotumiwa na mtu nje ya Uingereza na bara la Ulaya haijumuishi ujumbe mfupi, simu au makundi.

Taarifa hizo ni:

  • Namba ya simu na taarifa za usajili kama jina
  • Taarifa za simu anayotumia mtumiaji wa huduma yao kwa mfano simu ya kampuni gani?
  • Kampuni inayompa mtandao mtumiaji
  • Malipo anayoyafanya kwa kutumia WhatsApp



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages