MBUNGE wa Jimbo la Rorya mkoani Mara, Jafari Wambura Chege, leo Februari 8, 3021 ameshiriki kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri na kuwataka madiwani kuishauri halmashauri hiyo kubuni vyanzo vya mapato vilivyo imara kwa ajili ya kumudu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wanandi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Chacha, kikao hicho ni cha bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2021/2022.
![]() |
Diwani wa Kata ya Nyamagaro, Ezra Masana (kulia) na madiwani wengine wakishiriki kikao hicho. |
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ng'ong’a Gerald, ambapo madiwani mbalimbali akiwamo Ezra Masana wa Kta ya Nyamagaro wamepata nafasi ya kuchangia masuala ya uboreshaji wa huduma za jamii.
#MaraOnlineNews-Updates
No comments:
Post a Comment