NEWS

Thursday 7 October 2021

Dereva basi la Zakaria lililosabisha ajali atakiwa kujisalimisha polisi kabla jua halijazama leo



MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Wilbrod Mutafungwa amemtaka dereva basi la Zakaria lililosababisha ajali Jumapili iliyopita katika kijiji cha Gamasara wilayani Tarime, kujisalimisha polisi leo kufikia saa 12 jioni.

SACP Mutafungwa ametoa agizo hilo, wakati alipotembelea eneo la ajali hiyo, ambapo Zakaria Air Bus lenye namba za usajili T 906 DLJ wakati likitoka mkoani Mwanza liligonga gari dogo aina ya Prado lenye namba T 184 AQT lililokuwa likitokea mjini Tarime na kusababisha vifo vya watu wawili.

“Ajali hii ilitokea baada ya dereva wa basi kuhama njia yake, kuvuka mstari mweupe wa barabarani unaozuia gari kubadili njia, huku akijua kuwa eneo hilo haliruhusiwi kufanya hivyo, kwa sababu lina kona na kulifuata gari dogo upande wa kulia kisha kuligonga na kusababisha ajali hiyo.

“Tunamtaka dereva huyo ajisalimishe kabla ya jua kuzama, tunajua kwamba alitoka mzima na kukimbia, hivyo ajisalimishe kabla ya jioni ya leo,” amesema SACP Mutafungwa.

SACP Mutafungwa akiwa eneo ambalo ajali ilitokea

Ameongeza kuwa endapo dereva huyo atashindwa kujitokeza baada ya muda huo, mmiliki wa basi hilo awe tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi kumtafuta, kwa sababu yeye ndiye alimwajiri, anajua taarifa zake sahihi.

Aidha, Mtafungwa amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri nchini kutunza kumbukumbu sahihi za wafanyakazi wao, ili wakifanya makosa na kukimbia taarifa hizo zitumike kuwatafuta, vingenevyo watawajibika wao.

(Na Mobini Sarya, Tarime)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages