NEWS

Monday 1 November 2021

Mkutano Mkuu WAMACU waridhia kufuta deni lililokosa vielelezo



CHAMA cha Ushirika wa Wakulima wa Mara Cooperative Union (WAMACU) kimefuta deni la shilingi zaidi ya milioni 275 zilizokuwa hatarini kuangukia kwenye mikono ya ‘wajanja’.

Maamuzi hayo yamefikiwa katika Mkutano Mkuu wa WAMACU, uliofanyika mjini Tarime Oktoba 29, 2021, chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo, David Hechei.


Wajumbe mkutanoni

“Baada ya wajumbe wa mkutano mkuu kuridhia, sasa vitabu vitapelekwa kwa Mrajis kwa ajili ya kufutwa,” Meneja Mkuu wa WAMACU, Samwel Kisiboye ameiambia Mara Online News, muda mfupi baada ya mkutano huo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Bodi ya WAMACU kufuatilia na kubaini hakuna vielelezo vinavyothibitisha uhalali wa deni hilo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Col. Michael Mntenjele ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, amehimiza suala la kuzingatia taratibu za ushirika kuhusu ununuzi wa kahawa.

DC Mntenjele (kushoto) akizungumza katika mkutano huo

“Wanunuzi wa kutoka nje ya chama wanaruhusiwa kufanya hivyo kwa kufuata sheria na sio kuwakopa wakulima, ili mwisho wa siku wakulima nao wapate tija ya jasho lao,” Mntenjele amesema.

Aidha, Mntenjele ametoa wito kwa wakulima hao kushirikisha vijana ili baadaye wawe waridhi wao wa kuendeleza uzalishaji wa zao hilo la biashara.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages