NEWS

Saturday 15 January 2022

Mkurugenzi Idara ya Maji akagua mradi wa maji Lindi, ataka ukamilishwe kabla ya Februari 2022



MKURUGENZI wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Wizara ya Maji, CPA Joyce Msiru (pichani juu katikati), leo Januari 15, 2022 amekagua maendeleo ya mradi wa maji Mwitero mkoani Lindi.

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji imewekeza shilingi bilioni 3.5 kugharimia mradi huo, ambao utekekezaji wake hadi sasa umefikia asimilia 85.



Mradi huo unatarajiwa kusambaza huduma ya maji safi kwa wananchi takriban 40,000 baada ya kukamilika.

“Maendeleo ya mradi ni mazuri lakini nimeitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Lindi kuhakikisha kuwa mradi unakamilika ifikapo mwisho wa mwezi huu [Januari 2022],” CPA Joyce amesema muda mfupi baada ya kukagua mradi huo.



Katika ziara hiyo, CPA Joyce alifuatana na Msaidizi wa Kitengo cha Utoaji Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Wizara ya Maji, Mhandisi Lidya Joseph.

(Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Lindi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages