MBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, leo Januari 28, 2022 ametoa shilingi milioni moja kuchangia sherehe za miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zitakazofanyika kitaifa mkoani Mara.
Fedha hizo ambazo zimekabidhiwa kwa uongozi wa jumuiya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Mara, zinafanya kiasi cha mchango uliotolewa na Mbunge Muhongo kwa ajili ya sherehe hizo kufikia shilingi milioni tano.
Profesa Sospeter Muhongo
Hivi karibuni, mbunge huyo aliipatia jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya CCM Mkoa wa Mara shilingi milioni moja, kisha shilingi milioni tatu kwa CCM Mkoa.
Mwakilishi wa Mbunge Muhongo, Mboi Kahinda (kushoto) akipokea stakabadhi ya mchango huo kutoka kwa Katibu wa UVCCM Mara, Wambura Pelesia Igembya.
#MaraOnlineNews-Updates
No comments:
Post a Comment