NEWS

Sunday, 1 February 2026

Hakuna mpango wa BoT kuuza dhahabu kugharimia miradi ya serikali






Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
........................................

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema haina mpango wowote wa kuuza dhahabu ili kugharimia miradi ya serikali.

Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa benki hiyo, Emmanuel Akaro, alisema jijini Dar es Salaam juzi kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT imeidhinisha chombo hicho kikubwa cha fedha nchini kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili.

Alisema mpaka sasa thamani ya hifadhi ya dhahabu katika benki hiyo imefikia dola bilioni 3.24, ongezeko ambalo BoT imepanga kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoinishwa ili kusawazisha mizania ya hifadhi.

Akaro alisema hatua hiyo ni ya kawaida katika usimamizi wa akiba ya fedha za kigeni na haina uhusiano wowote na ufadhili wa miradi ya serikali.

Mkurugenzi huyo alitoa ufafanuzi huo kufuatia kuzagaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kwamba BoT ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu ili kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

"Madai hayo si ya kweli na hayana msingi," Akaro alisema

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages