NEWS

Friday 13 January 2023

Chandi aagiza sekondari mpya ifunguliwe kijijini Mrito, uboreshaji huduma za matibabu Nyamongo



Na Mwandishi Wetu, Tarime
-----------------------------------------

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (pichani), ameagiza kufunguliwa kwa shule mpya ya sekondari ambayo imejengwa katika kijiji cha Mrito wilayani Tarime.

Chandi alitoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Tarime na kupata fursa ya kuona shule hiyo ambayo asilimilia kubwa ya ujenzi wa majengo yake umekamilika.

“Naagiza hii shule ifunguliwe ili kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu, lakini pia kuepushia watoto wa kike vishawishi vinavyoweza kuwasababisha kupata mimba wanapokwenda kutafuta elimu kwenye shule jirani,” aliagiza bosi huyo wa chama tawala mkoani Mara.

Diwani wa Kata ya Kemambo, Rashid Bogomba ameiambia Mara Online News leo asubuhi kuwa maandalizi ya kufungua shule hiyo yapo hatua za mwisho.

“Kinachosubiriwa kwa sasa ni ukamilishaji wa vyoo na nyumba ya mwalimu na tunatamani sana shukle hii ifunguliwe mwaka huu na kuanza kupokea wanafunzi,” amesema Bogomba.

Wanafunzi ambao watatumia shule hiyo ni pamoja na wanaotoka katika maeneo ambayo yapo jirani na mto Mara.

“Ni kweli wanafunzi kwa sasa wa maeneo kama ya mto Mara wanatembea karibia kilomita 13 kwenda kusoma shule ya jirani ya Kerende,” amesema Bogomba ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime yenye utajiri mkubwa wa madini.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Chandi, amekitaka kituo cha afya Nyangoto - maarufu kwa jina la Sungusungu kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi na kuhakikisha huduma muhimu kama za X-ray na Ultrasound zinapatikana kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages