NEWS

Thursday 5 January 2023

RC Mzee apokea madarasa mapya 41 ya sekondari katika Halmashauri ya Tarime Mji, apongeza ubora wa viti na meza za wanafunzi



Na Mara Online News
----------------------------------

MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee (pichani juu kulia), amekagua na kupokea vyumba vipya vya madarasa ya shule za sekondari vipatavyo 41, vyenye thamani ya shilingi milioni 820 katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Akizungumza wakati wa ziara yake jana, RC Mzee aliipongeza Halmashauri hiyo kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo na kutengeneza viti na meza vyenye ubora kwa ajili ya wanafunzi.



Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Gimbana Ntavyo (pichani juu kabisa kushoto), alimueleza Mkuu huyo wa mkoa kwamba vyumba vya madarasa 41 vilivyokamilika vitachukua wanafunzi wote 3,480 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wa 2023.

Mbali na vyumba hivyo, Mkurugenzi Ntavyo alisema Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wananchi, imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa shule mbili mpya za sekondari; mbazo ni Ikoro iliyopo kata ya Turwa na Magena katani Nkende.

Shule hizo, alisema zitawapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kwenda masomoni na kurudi nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages