NEWS

Saturday 27 May 2023

DC Mashinji awahimiza madiwani Serengeti kuhamasisha wafanyabiashara kuchangia usafi wa mji wa Mugumu

Mkuu wa Wilaya, Dkt Vincent Mashinji (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti jana.

Na Mwandishi Wetu, Serengeti
-------------------------------------------------

MKUU wa Wilaya (DC) ya Serengeti mkoani Mara, Dkt Vincent Mashinji, amewahimiza madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kuhamasisha - badala ya kugomesha wafanyabiashara kuchangia gharama za usafi wa mji wa Mugumu.

“Kama huwezi kupata shilingi 200 ya kuzoa takataka funga duka, unapoteza muda mjini… kuna madiwani wanapita mtaani wanasema msikubali,” alisema DC Mashinji katika kikao cha baraza la madiwani hao kilichofaanyika mjini Mugumu, jana Ijumaa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Serengeti, Mrobanda Japan aliwahimiza madiwani hao kushirikiana katika kuhakikisha fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kugharimia miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri hiyo zinatumika vizuri.
Mrobanda akizungumza kikaoni

“Nendeni mkaunde timu za ushirikiano, fedha hii anayoleta Mama Samia Suluhu Hassan [Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania] kufanya maendeleo ya wananchi, basi ifanye kile kilicho lengwa,” alisema Mrobanda.

Kikao hicho cha baraza la madiwani kiliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe kwa tiketi ya chama tawala - CCM.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages