NEWS

Thursday 29 February 2024

Waziri Mkuu Majaliwa aweka jiwe msingi jengo la Halmashauri ya Wilaya Musoma, Prof Muhongo amkabidhi vitabu vinavyoonesha wanavyotekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (wa pili kulia), ameweka jiwe la msingi katika jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma leo Februari 29, 2024. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo na viongozi wengine wakifurahia tukio hil

Prof Muhongo alimweleza Waziri Mkuu kwamba Musoma Vijijini ni jimbo bora kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano inaoendelea kumpa katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kisekta.

Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo pia kumkabidhi Waziri Mkuu Majaliwa nakala za vitabu vinavyoonesha Ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo katika jimbo la Musoma Vijijini.

Muonekano wa mbele wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
------------------------------------
Waziri Mkuu Majaliwa yupo katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara kwa siku ya tano leo, ambapo ameweza kufika katika wilaya zote sita za mkoa huo kukagua, kuzindua, kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo, kuzungumza na viongozi, kuhutubia mikutano ya hadhara, kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maagizo ya ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages