NEWS

Wednesday 3 July 2024

Rais Samia afanya mabadiliko ya uongozi Wizara za Viwanda, Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais, TRA



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
-----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
---------------------------

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt Selemani Jafo ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa Dkt Jafo amechukua nafasi ya Dkt Ashatu Kachwamba ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Aidha, Rais Samia amemteua Mhandisi Yahaya Ismail Samamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini, akichukua nafasi ya Kheri Abdul Mahimbali ambaye kwa mujibu wa taarifa hiyo, atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Samamba alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amemteua Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kabla ya uteuzi huo, Mwenda alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).

Naye Alphayo Japan Kidata ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mshauri wa Rais, Ofisi ya Rais - Ikulu. Kabla ya uteuzi huo, Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA, ilieleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu, Sharifa Nyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages