Na Mwandishi Wetu
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa mwongozo na maelekezo kwa wanachama wake kuhusu utaratibu wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu kuomba kuteuliwa kugombea uongozi wenye vyombo vya Dola katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba 2025.
“Ni marufuku kwa mwanachama yeyote kualika kundi la wapembe kumsindikiza kwenda CCM kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea,” imesema taarifa ya CCM na kuongeza:
“Ni marufuku kwa mwanachama kuandaa msafara wa magari, pikipiki, baiskeli, ngoma na matarumbeta ya kumsindikiza kwenda CCM kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea.”
Taarifa hiyo kwa umma iliyotolewa Juni 25, 2025 na kusainiwa na Katibu wa NEC Organaizesheni, Issa Haji Ussi (GAVU), kwa lengo la kusimamia na kulinda misingi ya chama hicho katika kuwaunganisha wanachama wake ili kuimarisha umoja, upendo, ushirikiano na mshikamano.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na CCM, mchakato wa ndani wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kugombea uongozi katika vyombo vya Dola nchini utaanza rasmi kesho Juni 28, 2025.
No comments:
Post a Comment