NEWS

Monday, 18 August 2025

Mwenge wa Uhuru 2025 wawasha Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa Baba wa Taifa wilayani Butiama




Na Mwandishi Wetu, Butiama

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, jana Agosti 18 aliongoza tukio la Mwenge huo kuwasha Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarege Nyerere, wilayani Butiama, Mara.

Tukio hilo la kuwasha Mwenge wa Mwitongo ni la 61 tangu Mbio za Mwenge wa Uhuru zianzishwe mwaka 1964 nchini.


Katika tukio hilo, Ussi aliambatana na wakimbizaji wengine kadhaa wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa, wazee wa kimila na familia ya Mwalimu Nyerere.

Wakiwa nyumbani hapo kwa Baba wa Taifa, viongozi wa mbio hizo za Mwenge wa Uhuru walipata taarifa za kihistoria kuhusu Mwenge wa Mwitongo, Baba wa Taifa na familia yake, kuzuru kaburi lake na kuweka mashada, kisha kutembelea Makumbusho ya Mwalimu Julius K. Nyerere.



Nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwenge ulipokewa na wanafamilia wa Mwalimu Nyerere wakiongozwa na kiongozi wa familia hiyo, Chifu Japheti Wanzagi, ambaye pia ni kiongozi wa kabila la Wazanaki.


Aidha, Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Butiama ulitembelea miradi minane ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.767, kati ya hizo fedha za wananchi ni shilingi bilioni 1.288, mchango wa Halmashauri ya Wilaya (shilingi milioni 45) na Serikali Kuu (shilingi bilioni 2.433).

Leo Agosti 19, Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 zinafanyika katika wilaya ya Rorya, mkoani Mara.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages