
Na Mwandishi Wetu, Musoma
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya mafuriko, ikiwa ni pamoja na kuepuka kutupa takataka kwenye mitaro na kujenga makazi kwenye mikondo ya maji.
Chikoka alitoa maelekezo hayo jana alipokwenda kujionea mafuriko yaliyozikumba kata za Bweri, Rwamrimi na Nyakato, ambapo nyumba 10 zilizingirwa maji na wakazi zaidi ya 30 kunusurika kifo.
Hata hivyo, alisema mamlaka za serikali zinashughulikia uboreshaji wa miundombinu ya njia katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment