
Na Joseph Maunya
Mara
---------

Mzee wa Kimila na mkazi wa kijiji cha Kegonga, Kiruka Wantahe, akizungumza kwenye tamasha.

Viongozi wakikabidhi zawadi kwa wanafunzi walioshinda kwenye tamasha.

Charles Mashauri akizungumza katika tamasha lililofanyika kijijini Kegonga.

Daniel Fungo akizungumza kwenye tamasha.
Mara
---------
Imeelezwa kuwa elimu inayotolewa na Kanisa la AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Right to Play, imesaidia kuchochea mwitikio wa jamii katika wilaya za Tarime na Serengeti kutambua umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.
Wazazi na viongozi mbalimbali waliyasema hayo wiki iliyopita walipohudhuria matamasha ya michezo ya uhamasishaji juu ya umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike yaliyoandaliwa na taasisi hizo kwenye maeneo tofauti katika wilaya hizo.

Mzee wa Kimila na mkazi wa kijiji cha Kegonga, Kiruka Wantahe, akizungumza kwenye tamasha.
"Kwa sasa hatuna sababu za kutosomesha watoto wa kike, pia naomba sana muendelee kuwa karibu na sisi na kutuelimisha zaidi," alisema Kiruka Wantahe, Mzee wa Kimila kutoka kijiji cha Kegonga, kata ya Nyanungu wilayani Tarime.
"Kwa kweli mwitikio kwetu sisi umekuwa ni mkubwa na watoto wa kike wanapelekwa shule, na hata wao pia wamejitambua - wanapambana na matukio ya ukatili kama ukeketaji kwa kukimbilia kituo cha afya," alisema Lucia Paulo Yusufu, mkazi wa kijiji cha Kegonga wakati wa tamasha lililofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kegonga.

Viongozi wakikabidhi zawadi kwa wanafunzi walioshinda kwenye tamasha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi kutoka AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe, Charles Mashauri, aliwashukuru wakazi wa kata ya Nyanungu kwa kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu inayotolewa na taasisi hizo tofauti na zamani ambapo mahudhurio yalikua hafifu.
"Niwashukuru sana wazazi na walezi kwa kuhudhuria - maana kipindi cha nyuma tulikuwa tunaona wanafunzi ni wengi kuliko wazazi, lakini leo wazazi mko wengi kiasi kwamba huu ujumbe wetu juu ya umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike utafika mbali zaidi na kwa urahisi," alisema Mashauri.

Charles Mashauri akizungumza katika tamasha lililofanyika kijijini Kegonga.
Katika wilaya ya Serengeti, tamasha la uhamasishaji lilifanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Wagete, ambapo Afisa Mtendaji wa Kata ya Rigicha, Kimori Moremi, alisema ujumbe wa taasisi hizo umeleta mwitikio mkubwa kwa wakazi wa huko.
"Mwitikio wa jamii yetu umekuwa mzuri maana kwa sasa idadi ya watoto wa kike katika shule zetu imeongezeka, matukio ya ukatili dhidi yao yamepungua, na hiyo inamaanisha kwamba elimu mnayowapa inawafikia vyema, hivyo niwaombe muendelee na msichoke," alisema Kimori.
Naye Afisa Mradi mwingine kutoka AICT, Daniel Fungo, alisema taasisi hizo zinashirikiana kutoa elimu kwa jamii katika wilaya za Tarime na Serengeti mkoani Mara juu ya umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike, chini ya mradi wa Save Her Seat (Linda Kiti cha Mtoto wa Kike) wakilenga kufikia shule 20 kwa kila wilaya.

Daniel Fungo akizungumza kwenye tamasha.
No comments:
Post a Comment