![]() |
Butiku Masaku Mwita "Kapanya" |
Na Godfrey Marwa
Tarime
-------------
Tarime
-------------
Katika hali ambayo ni nadra kutokea, mgombea nafasi ya udiwani kata ya Sabasaba katika jimbo la Tarime Mjini kupitia CHAUMMA, Butiku Masaku Mwita - maarufu kwa jina la Kapanya, ameweka wazi msimamo wake wa kuwanadi wagombea wa ACT Wazalendo katika maeneo ambayo chama chake hakikusimamisha wagombea kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba 29, 2025.
Kapanya ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHAUMMA Wilaya ya Tarime, aliyasema hayo wakati alipotembelea ofisi za Mara Online News, mjini Tarime jana Septemba 28, 2025.
"Ninasimama kwenye majukwaa ya ACT kwenye maeneo ambayo hatuna mgombea, sisi CHAUMMA tunaungana na ACT ili kuiondoa Serikali ya CCM madarakani kwa kunadi sera ambazo zenye uwezo wa kufanya taifa hili lifike sehemu ambayo Watanzania wanatarajia.
"Nitaendelea kusimama katika majukwa ya ACT kunadi ACT jimbo la Tarime Vijijini kumwombea mgombea ubunge kura pamoja na kwenye kata zote zenye wagombea udiwani wa ACT.
"Pale ambapo nimeweka wagombea udiwani katika jimbo la Tarime Vijijini siwezi kusimama na kuomba kura… Tumekubaliana na chama cha ACT Wazalendo na viongozi wao kwamba tutaungana tukifanya mikutano mjini,” alisema Kapanya.
No comments:
Post a Comment