
Mkurugenzi wa Chichake Sports Bar & Grill, Nicolous Chichake (aliyevaa kaunda suti), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wageni mbalimbali wakisherekea mwaka moja wa uwekezaji huo.
Na Mwandishi Wetu
Tarime
-----------
Mji wa Nyamongo umeendelea kushuhudia mageuzi makubwa ya maendeoleo katika miaka ya hivi karibuni, shukurani kwa wadau wote wanaochangia kukua kwa mji huo ambao upo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.
Ni ukweli usiopingika kuwa Nyamongo ya leo sio Nyamongo ya miaka ya 2010 na kurudi nyuma, kuna maendeleo mengi yanaonekana katika eneo hilo ambalo limebarikiwa kuwa na ukwasi mkubwa wa dhabahu.
Wakazi wa mji huo wameendelea kujenga majengo ya kisasa ya makazi na biashara mbalimbali.
Aidha, wadau wengine ikiwemo serikali na mgodi wa North Mara nao hawajabaki nyuma katika kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma za kijamii kama vile maji, elimu na barabara katika vijiji vinavyozunguka mgodi huo.
Mmoja wa wadau wa maendeleo ambaye ameweka alama katika kuchangia maendeleo ya ukuaji wa mji mdogo wa Nyamongo ni Nicolaus Chichake - baada ya kuwekeza kwenye sekta utalii na burudani.
Hivi sasa, Chichake anamiliki Chichake Sports Bar & Grill ikiwa ni sehemu maalum kwa ajili watu kupumzika na kuburudika huku wakipata vinywaji na chakula.

Mkurugenzi wa Chichake Sports Bar & Grill, Nicolous Chichake, akizunguma katika sherehe ya mwaka mmoja wa mradi huo.
Chichake Sports Bar & Grill imekuwa ni chaguo kwa wenyeji na wafanyakazi wa mgodi wa North Mara ambao wamekuwa wakikosa huduma kama hizo katika mji wa Nyamongo kwa miaka ya nyuma na hivyo kulazimika kusafiri kwenda kuzitafuta nje ya mji huo.
"Mbali na wenyeji, wateja wetu wengi ni wafanyakazi wa mgodi wa North Mara, lakini pia tunapata wageni kutoka nje ya mkoa wetu wa Mara,” anasema Chikake katika mahojiano maalum na Gazeti la Sauti ya Mara wiki iliyopita.
Septemba 16, 2025, Chichake Sports Bar & Grill ilisherehekea ‘Birth Day’ yake ya mwaka mmoja tangu ilipofungua milango kwa wateja wake.
“Tunataka tuwahakikishie wateja wetu huduma bora zaidi ndani ya Chichake Sports Bar & Grill. Tunataka kuwa the ‘best’, yaani eneo bora la burudani katika ya mkoa wetu wa Mara,” Chichake alisema katika sehemu ya hotuba yake kwenye sherehe ya mwaka moja wa Chichake Sports Bar & Grill.
Chichake Sports Bar & Grill ipo umbali wa takriban kilomita tatu kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti kupitia lango la Lamai. Hivyo, ni sehemu sahihi kwa watalii wa ndani na nje kupumzika wanapokuwa wanatembelea hifadhi hiyo bora Afrika wakiwa wilayani Tarime.
Mbali na kuwa sehemu ya kuburudika, uwekezaji huo wa Chichake Sports Bar & Grill umetengeneza ajira za moja kwa moja na ambazo sio za moja kwa moja kwa vijana.
Chichake pia anawashukuru wateja na wadau wao wote wanaochangia uendelevu wa biashara hiyo, huku akiwaahidi huduma bora zaidi, ikiwemo usalama wa wateja wao saa 24.
Chichake amekuwa marufu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ubunifu katika biashara zake ambazo zinaelezwa kugusa maisha ya vijana walio wengi, hasa kwenye upande wa ajira.
“Kwa sasa hivi, Chikake Sports Bar & Grill tuna wafanyakazi 62 kutoka maeneo mbalimbali, na mwakani tutaongeza ajira kwa sababu tunaenda kuongeza wigo wa kibiashara,” alisema Chichake.
Nicolaus Chichake ni msomi wa Chuo Kikuu Kikuu na mmoja wa wakandarasi wazawa ambao wana kamapuni ambazo zinapata fursa za kibiashara katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara, ikiwa ni sehemu ya matunda ya Ushirikishwaji wa Watanzania yaani ‘Local Content’.
Wafanyakazi wa Chikake Sports Bar & Grill wanamshukuru Mkurugenzi wao [Nicolous Chichake] kwa kufanya uwekezaji huo, huku wakiahdi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao.

No comments:
Post a Comment