
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, akiwasilisha taarifa ya wizara hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - marufu kwa jina la NUU, jijini Dodoma jana JUmatatu.
Dodoma
---------------
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - maarufu kwa jina la NUU.
Waziri Nyansaho ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, alikutana na Kamati hiyo katika ofisi za Bunge jijini Dodoma, jana Januari 19, 2026 kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya wizara hiyo.

Kikao hicho kati ya Waziri Nyansaho na kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Najma Murtaza Giza na Makamu Mwenyekiti wake, Pascal Inyasi Chinyele, kilihusisha kamati hiyo ya Bunge kupewa taarifa ya majukumu na muundo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Dkt. Nyansaho aliteuliwa Novemba 17, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

No comments:
Post a Comment