NEWS

Thursday, 1 January 2026

Watanzania tujipange kusonga mbele mwaka 2026




Na Mwandishi Wetu

Watanzania, kama walivyo watu wengine duniani kote, leo tunauanza mwaka mpya 2026 kwa shangwe tukikumbuka kwamba ustawi wa taifa letu nguzo yake kubwa ni haki, amani, umoja na mshikamano.

Hizo ndizo nguzo alizoziacha muasisi na Baba Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akiondoka madarakani mwaka 1985.

Ni tunu ambazo viongozi wote waliomfuata Mwalimu Nyerere wamezipigania kuzilinda hadi leo tunapofikia mwaka huu 2026.

Kwa miaka yote zaidi ya 60, Watanzania wa tabaka zote katika jamii tumeilinda nchi yetu kwa umoja na mshikamano na kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kila sekta.

Kwa mwaka huu 2026, tunatakiwa kujipanga zaidi ili kupitia umoja wetu tuweze kushinda vikwazo vya maendeleo yetu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages