NEWS

Wednesday, 20 May 2026

Prof Muhongo achaguliwa Makamu wa Rais wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Sayansi Afrika kwa Nchi za Afrika Mashariki




Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo


Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Musoma Vijijini na mwanazuoni maarufu nchini, Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, anechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Sayansi Afrika (AAS) kwa kipindi cha miaka mitatu 2026-2029 kwa nchi za Afrika Mashariki.

Taarifa kutoka Ofisi ya mwanazuoni huyo imeeleza kuwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika kwa njia ya kielektroniki yanaonyesha kuwa kura za "Ndiyo" alizopata Prof Muhongo ni 168, kura za "Hapana" mbili (2) na kura za "Kujizuia" 15, huku asilimia ya kura zilizopigwa ikiwa 74.60.

Prof Muhongo ni msomi mwenye wasifu ulioshiba anayetambulika kimataifa kama mwanasayansi maarufu.

Ana shahada ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Ufundi cha Berlin, Ujerumani.

Hapa nchini Tanzania amewahi kushika wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Chama cha Jiolojia Afrika na Mwanachama wa Chuo Kikuu cha Sayansi Afrika.

Pia ni Mwanachama wa Heshima wa Vyama vya Jiolojia vya London na Marekani na Mtafiti wa Heshima wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Jiolojia cha China.

Hali kadhalika, Prof Muhongo alikuwa Mkurugenzi wa Kanda Mwanzilishi wa wa Afrika wa Baraza la Kimataifa la Umoja wa Vyama vya Sayansi (ICSU).

Pia msomi huyo ni Mhariri Mkuu wa Jarida la African Earth Sciences, Elsevier, na Makamu wa Rais wa zamani wa Tume ya Ramani ya Jiolojia ya Dunia (CGMW).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages