NEWS

Sunday, 14 June 2026

Benki Kuu ya Tanzania yasherehekea miaka 60 ya kuimarisha sekta ya fedha, kukuza uchumi



Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki maadhimisho ya Miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
--------------------

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), iliyoanzishwa miaka 60 iliyopita, imepata mafanikio makubwa kwa kuwa chombo madhubuti kilichosimamia sekta ya fedha na kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa.

Ukweli wa mchango BoT wa kujenga sekta endelevu ya fedha ulibainika mwishoni mwa wiki, wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 1966.

BoT ilianzishwa miaka mitano baada ya uhuru wa Tanzania Bara na miaka miwili baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika umri wake wa miongo sita, BoT imesimamia kwa umahiri mkubwa ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Kazi kubwa iliyofanywa na BoT kukuza sekta ya fedha na kuimarisha uchumi ndiyo iliyomfurahisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 60 ya benki hiyo, yaliyofanyika Juni 12, 2026 jijini Dar es Salaam.

Rais Samia aliitaka kuimarisha uwezo wa kung'amua mwelekeo wa kiuchumi kitaifa na kuhakikisha wananchi wa kawaida wanapata taarifa sahihi za kifedha kwa lugha inayoeleweka.

Pia, Rais aliitaka BoT kuhakikisha kuwa taasisi za kifedha zinaacha kutegemea dhamana za mikopo ambazo wananchi wengi hawana.

Aidha, alisisitiza kwamba kuelekea utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, BoT haina budi kuimarisha akiba ya fedha za kigeni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages