NEWS

Monday, 29 June 2026

IGP Wambura ampandisha ACP Twaha kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora



IGP Camillus Wambura

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Twaha Juma Lulengelule aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa (RCO) wa Tabora kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) huo.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jeshi hilo leo Jumatatu, Juni 2026, imeeleza kuwa uhamisho huo wa ACP Twaha umefanyika kujaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa RPC wa Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard George Abwao kufariki dunia Juni 20, 2026.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages