NEWS

Friday, 26 June 2026

IGP Wambura, RC Mtambi washiriki mazishi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Tabora SACP Abwao



IGP Camillus Wambura akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi walipokutana katika mazishi ya aliyekuwa RPC Tabora, SACP Richard Abwao, wilayani Rorya leo.

Na Mwandishi Wetu
Rorya
-------------

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura, ameungana na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, kushiriki mazishi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard George Abwao.

Kanali Mtambi akisaini kwenye kitabu cha maombolezo msibani hapo.

Mazishi hayo yamefanyika leo Juni 26, 2026 katika eneo la Nyatike lililopo Shirati, wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Baadhi ya viongozi wengine walioshiriki mazishi hayo ni IGP Mstaafu Simon Sirro ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi, Wakuu wa Mikoa, Paul Chacha (Tabora) na Anthony Mtaka (Njombe).


Mwenyekiti Chandi akisaini katika kitabu cha maombolezo msibani hapo.

SACP Abwao alifariki dunia Juni 20, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages