
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa mjini Musoma jana.
Musoma
---------------
Mkoa wa Mara umepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya chama tawala - CCM, ambapo miradi 315 yenye thamani ya shilingi bilioni 422.77 imetekelezwa katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi kuanzia Julai 2025 hadi Mei 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, aliwasilisha taarifa hiyo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kilichofanyika Juni 25, 2026 mjini Musoma na kubainisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 87.5.

Sehemu ya wajumbe kikaoni
Kanali Mtambi alisema mkoa huo unaendelea kufuatilia miradi mikubwa ya kimkakati iliyomo katika Ilani ya CCM ya mwaka 2025-2030, ikiwemo ujenzi wa reli ya SGR kutoka Tanga hadi Musoma; ukarabati na upanuzi wa Bandari ya Musoma na ujenzi wa reli ya SGR kutoka Simiyu hadi Musoma.
Miradi hiyo imegusa sekta muhimu zikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu ya usafiri ili kuboresha huduma za kijamii, kuongeza fursa za ajira, kukuza uzalishaji na kuimarisha ustawi wa wananchi mkoani Mara.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi, alisema chama hicho kitaendelea kuisimamia na kuishauri serikalini ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kama iliyoainishwa kwenye ilani hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi, akizungumza katika kikao hicho. (Picha zote na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment