NEWS

Sunday, 14 June 2026

Waziri Aweso hakuna kulala usakaji suluhu ya ukosefu wa huduma ya maji Mwanza



Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (kushoto), akiongoza kikao na Menejiment ya MWAUWASA jijini Mwanza, mapema leo.

Na Mwandishi Wetu
Mwanza
--------------

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amefika mkoani Mwanza mapema alfajiri ya Juni 15, 2026 na kuanza kazi ya kuimarisha huduma ya maji kwa wakazi wa jiji la Mwanza.

Waziri Aweso amefika katika kituo cha kusukuma maji cha Capri-point na kuongoza kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), kabla ya kukagua hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi.

Waziri Aweso akikagua mitambo ya kusukuma maji katika kituo cha Capri-point

Dhamira ya waziri huyo ni kupata picha halisi ya hali ya huduma ya majisafi, kubaini changamoto zilizopo na kuandaa mpango wa hatua za haraka na za kudumu za kuboresha huduma hiyo.

Waziri Aweso amewataka wataalamu wa Wizara ya Maji na MWAUWASA kukesha wakifuatilia na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji unaimarika jijini Mwanza.

Aidha, Waziri Aweso ameahidi kutembelea maeneo kadhaa kujionea hali halisi, ikiwemo chanzo kikuu cha maji cha Butimba mchana wa leo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages