
Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kesho Jumatatu anatarajia kuanza ziara ya kukagua hali ya upatiikanaji wa huduma ya maji mkoani Mwanza na utekelezaji wa miradi katika sekta hiyo.
Waziri Aweso ataitumia fursa hiyo pia kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kubuni mbinu za kuboresha huduma hiyo mkoani Mwanza
Lengo kubwa la Wizara ya Maji ni kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama mijini na vijijini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment