
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
--------------------


Dar es Salaam
--------------------
Mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji vitabu maarufu nchini, Nyambari Nyangwine, ametoa na kukabidhi zawadi ya vitabu na vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 50.63 kwa Shule ya St. Anne Marie ya jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo ni vya wanafunzi wa elimu ya awali (chekechea), darasa la kwanza hadi la saba na kidato cha kwanza hadi cha nne, sambamba na mipira ya michezo.
Nyambari amekabidhi zawadi hiyo leo Julai 18, 2026, wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 25 ya shule hiyo, mgeni rasmi akiwa Prof. Anna Tibaijuka.

Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) akikabidhi sehemu ya zawadi hiyo ya vitabu na mipira ya michezo.
Nyambari ametumia fursa hiyo pia kuhamasisha wazazi, wamiliki wa shule, wanafunzi na wadau wengine wa sekta ya elimu kushirikiana kwa kwa hali na mali katika kuwezesha watoto wa Kitanzania kupata elimu ubora.
Amesisitiza pia umuhimu wa kuongeza ubunifu katika ufundishaji ili kuwapa wanafunzi maarifa na stadi zinazowaandaa kujiajiri baada ya kuhitimu masomo, badala ya kuwaza kuajiriwa pekee.

“Tushikamane kuinua elimu yetu ya Tanzania. Shule binafsi na za serikali tujitahidi kwa kila linalowezekana tutoe elimu kwa vitendo na tuandae vijana wetu wawaze kujiajiri na siyo kuajiriwa,” amesema Nyambari.
Nyambari Nyangwine ambaye pia ni mwanasiasa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime kwa tiketi ya chama tawala - CCM, amekuwa akigawa misaada ya vitabu vya kiada na ziada katika maeneo mbalimbali Tanzania kupitia tasisi yake ya Nyambari Nyangwine Foundation, ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za serikali katika kuinua taaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi nchini.
No comments:
Post a Comment