
Kamishna mpya wa Uhifadhi TANAPA, Massana Mwishawa.
Dar es Salaam
---------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Massana Gibril Mwishawa kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Bosi huyo mpya wa TANAPA anachukua nafasi ya Mussa Nassoro Kuji ambaye amemaliza muda wake.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ilieleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Mwishawa alikuwa Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara wa shirika hilo.
“Uteuzi huu unaanza mara moja,” ilihitimisha taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu.
TANAPA inasimamia Hifadhi za Taifa 21 nchini.
No comments:
Post a Comment