NEWS

Wednesday, 8 July 2026

Sekondari za juu Musoma Vijijini kuanza mashindano ya Mbunge wa Jimbo



Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo.

Na Mwandishi Wetu
Musoma
---------------

Shule nne za sekondari za juu ((high schools) katika jimbo la Musoma Vijijini zitaanza rasmi mashindano yaliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo, Prof. Sospeter Muhongo, kuhusu uelewa na ufaulu wa wanafunzi wa shule hizo.

Mashindano hayo, ambayo yatakuwa na zawadi kwa washindi, yatafanyika mwezi ujao, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Mbunge huyo iliyotolewa mapema wiki hii.

Shule zitakazohusika na mashindano hayo ni Kasoma, Suguti, Mugango na Mtiro.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo ilieleza kuwa Jumamosi ijayo wanafunzi watakaoshiriki watapewa ng’ombe mmoja wa kitoweo.

Katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita 2026, asilimia 91.92 ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kasoma, yaani wanafunzi 198 walifaulu daraja la kwanza huku asilimia 8.08 (wanafunzi 16) wakifaulu daraja la pili.

Shule hiyo ni ya mchepuo wa masomo ya Historia, Jiografia na Fasihi, Kiswahili na Fasihi, Jiografia na Kiswahili.

Lengo kubwa la jimbo la Musoma Vijijini ni kuwa na shule za juu za sekondari 10 za masomo ya sayansi ifikapo mwaka 2030.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages