
Sehemu ya wafanyakazi wanawake wa Mgodi wa Dahabu wa Barrick North Mara wakati wa maadhimisho ya siku yao jana.
Tarime
--------------
Wafanyakazi wanawake wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara na wenzao kutoka kampuni za wakandarasi wazawa wa mgodi huo, wameeleza kufurahishwa na juhudu zinazofanywa na kampuni ya Baririck katika kuwapatia fursa za ajira na kuwaboreshea mazingira ya kazi bila ubaguzi.
Wanawake hao walitoa shukrani hizo wakati wa sherehe yao ya kuadhimisha Siku ya Wanawake katika sekta ya madini duniani, iliyofanyika usiku Julai 4, 2026, kwenye ukumbi wa Social Hall ndani ya mgodi huo unaoendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals.
Sherehe ya maadhimisho hayo yaliyokuwa na kaulimbiu ya “Women Taking Over”, ilihudhuriwa pia na baadhi ya wanawake wabobezi kwenye sekta ya madini waliofanikiwa kushika nafasi za uongozi kazini, ambao pia walionesha kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na mgodi huo kuvutia na kuwezesha wafanyakazi wanawake.

“Hili ni jambo kubwa sana, na hii sio tu siku ya wanawake, bali nguvu ya wanawake inayoonekana kwenye uzalishaji na usalama,” alisema Zuwena Senkondo kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ambao pia unaendeshwa na Barrick-Twiga.
“Leo ni siku maalum kwetu kama wafanyakazi wanawake katika sekta ya madini. Tunafurahi Barrick kutupatia kazi na fursa kama hii ya kukutana na kufurahi pamoja,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa mgodi huo huku akionesha tabasamu kubwa.
Mfanyakazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bhoke Juma kutoka kampuni ya AKO ambayo ni mkandarasi katika mgodi huo, alisema Barrick ni mfano wa kuigwa katika kujali wafanyakazi wake.
“Tungependa kuona kampuni za wakandarasi nazo zinajifunza mambo mazuri kama ambayo Barrick inawafanyia wafanyakazi wao wa kike,” alisema Bhoke.
“Barrick wanawapa wanawake kipaumbele kwenye fursa za kibiashara, inatuhamasisha kujitokeza kuchangamkia fursa za kazi za ajira na biashara mgodini,” alisema Lucy ni Mkurugenzi wa LUMRY General Supply.
Aliongeza: “Mbali na kunipa tenda za kufanya kazi mbalimbali kama vile kupamba na kutoa huduma ya chakula, Barrick wamenitangaza hadi nimeanza kupata kazi kubwa za kupamba matukio makubwa yakiwemo ya kiserikali na wanapenda kuona wanawake tunapata fursa na kuwa na mafanaiko makubwa.”
Lucy aliungana na wanawake wenzake kujipongeza kwa sherehe yao hiyo akisema imekuwa ya kihistoria, huku akishauri iwe endelevu.
Naye mfanyakazi wa mgodi wa North Mara, Neema Sokia, ambaye anaendesha mitambo katika uchimbaji madini chini ya ardhi (underground mining), alimshukuru Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko, kwa juhudi kubwa anazofanya kuhakikisha kuwa idadi ya wanawake katika mgodi huo inaendelea kuongezeka.
“Sasa hivi wanawake tuko wengi hapa North Mara japokuwa bado hatujafikia kiwango kinachotakiwa, ila General Manager (Meneja Mkuu) ametusaidia sana, tunapaza sauti tunasikika tunasikilizwa,” alisema Neema.
Akizungumza katika sherehe hiyo, Meneja Mkuu, Apolinary Lyambiko, alissiitiza umuhimu wa utekelezaji wa sera za kuhakikisha kuwa wanawake wengi wanapata fursa ya kushiriki katika ukuaji wa sekta ya madini.
GM Lyambiko akizungumza katika sherehe hiyo
“Hatupo hapa tu kusherehekea tukio la wanawake, lakini pia kuondoa vikwazo. Ushiriki wao katika sekta ya madini ni sehemu ya wajibu wetu,’ alisema GM Lyambiko ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Alitumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa wakandarasi wa Barrick North Mara kuendelea kuwezesha wafanyakazi wanawake na kuwajengea mazingira rafiki ya kazi muda wote.

Awali, akisoma risala yake kwa mgeni rasmi, Meneja Mahusiano Msaidizi wa Barrick North Mara, Nasieku Kisambu, alisema program ya maadhimisho hayo ilianza Juni 1, 2026 na kuhitmishwa jana, wanawake hao waliweza kupata mafunzo yakiwemo ya kiusalama kazini, lakini pia na kutoka nje kwenda kugawa misaada mbalimbali kwa familia 60 zenye uhitaji 60 katika vijiji viivyo jirani namgodi huo.

Nasieku akisoma risala kwa mgeni rasmi
Pia, Nasieku alisema walitembelea Gereza la Wilaya ya Tarime na kugawa misaada ya mahitaji mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu wanawake.

Nasieku aliushukuru puongozi pia uongozi wa Barrick North Mara na katika ofisi za Dar es salaam kwa kile alichosema ni viongozi ambao wana mtazamo chanya wa maendeleo kwa wafanyakazi wanawake.




No comments:
Post a Comment